Serikali imeombwa kuwaunga mkono wadau mbalimbali wa michezo, wakiwemo JACMA Mining & Service inayofadhili vijana kushiriki mbio za Marathon nchini.
Msimamizi wa JACMA Mining & Services JOGGING Club Sylivia Lushokana, amewasilisha ombi hilo, baada ya klabu hiyo kufadhili vijana ishilini kushiriki mbio za Shycom Alumni Marathon, zilizofanyika mkoni Shinyanga.
Mratibu wa mbio za Shycom Alumni Marathon Jackson Busilu, ameishukuru kampuni ya Kampuni ya JACMA Minning & Service kwa kushiriki mbio hizo.
Mbio za Shycom Alumni Marathon zimewashikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali nchini.