Katika kuhakikisha anaendelea kuingua mkono Serikali kwenye Sekta ya elimu na utoaji wa elimu bora na yenye kuleta tija kwa watoto wa Kitanzania Mkurugenzi wa Shule ya Santa Edwin English Medium School iliyopo Kata ya Mkolani Jijini Mwanza Bw.Edwin Soko amesema kuwa atahakikisha anaendelea kuisaidia jamii kwa kuendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kupitia mpango maalumu uliowekwa na uongozi shuleni hapo.
Soko ameyasema hayo Septemba.21,2024 katika mahafari ya kwanza ya Darasa la Saba ya shule hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Santa.Edwin ambapo ameongeza kuwa hadi sasa kuna watoto takribani 20 ambao wanapata ufadhili wa masomo shuleni hapo huku lengo kubwa ikiwa ni kurudisha kwa jamii.
"Tuna watoto takribani 20 ambao wanapata ufadhili wa elimu bure shuleni kwetu na hii yote ni kurudisha kwa jamii kwani St.Edwin ni jamii"....Alisema
"Ndugu zangu wazazi mbegu hii tunayoipanda hii leo hapa Santa.Edwin English Mediam School naamini ipo siku tutatoa viongozi wakubwa sana kama Mawaziri,Wakurugenzi,Walimu ,Madaktari watalamu wa sekta mbalimbali cha msingi tuamini kwenye mchakato tukiamini tutafika kwani kila kitu ni malengo na kujituma kwa bidii"....Alisisitiza
Aidha katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amewasii wazazi na walezi kuendelea kuiamini shule hiyo kwani imekua ikifanya vizuri kitaaluma pamoja na malezi ambapo kwa mwaka huu katika mtihani wa utathimini(MOCK EXAMINATION) Shule hiyo imeshika nafasi ya 15 kati ya shule 151 za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na nafasi ya kwanza katika shule zilizopo kata ya Mkolani .
"Sio mwaka huu tu hata mwaka jana kwenye mtihani kama huu tulishika nafasi ya kwanza ukweli walimu wanajitahidi sana kuhakikisha watoto wanasoma na kuwapa maadili mema ya kiroho na kimwili ndio maana tumekuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo"....Alisema
Kwa upande upande wake Julius Magembe ambaye alikua mgeni rasmi katika mahafari hayo ametoa wito kwa wakurugenzi na wamiliki wengine wa shule binafsi kuiga mfano wa Santa.Edwin English Mediam School kwa kutoa ufadhili wa masomo kwani kufanya hivyo ni kurudisha heshima kwa jamii na kuwasaidia wazazi ambao hawana uwezo na wanatani watoto wao kusoma shule binafsi.
"Nimeambiwa kuna wanafunzi 20 wanasoma bure kwa ufadhili wa Mkurugenzi basi wewe ni sehemu muhimu sana kwa jamii ni jambo la kujivunia sana basi na shule nyingine za binafsi ziige mfano kutoka kwako"...Alisema
Aidha katika hatua nyingine Magembe ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika shule ambazo zipo jirani na maeneo yao ya makazi kwani kufanya hivyo kutawasaidia watoto kuepukana na adha ya kuamka mapema na kurudi nyumbani kwa kuchelewa na kufanya hivyo itampa mtoto unafuu wa kupumzika na kujihusisha na shughuli nyingine ikiwemo michezo kwajili ya kujenga afya ya akili na kimwili.
"Wazazi na walezi wengi hawapendi kuwapandisha magari watoto wao usiku usiku isipokua wanalazimika kufanya hivyo ili watoto wao waende wakapate elimu kwenye shule ambazo wanaona zinafaa hivyo basi kwa taaluma na matokeo ya shule hii ya Santa.Edwin naamini mwakani utapata wanafunzi wengi sana kikubwa endeleeni kutoa malezi na elimu bora"....Alisisitiza
Awali akisoma risasi mbele ya mgeni rasmi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Hassan Mussa Ibrahim amesema kuwa kwa mwaka ujao wa masomo wanatarajia kuanza kupokea wanafunzi wa bweni kwani hadi hivi sasa wameshakamilisha ujenzi wa bweni la kisasa kwaajili ya watoto wa kike na wanaendelea na ujenzi wa bweni la watoto wa kiume ambapo lipo katika hatua za mwisho kabla ya kukamilika .