Bina alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake mkoani Geita iliyolenga kusikiliza na kujadili changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. Alisisitiza umuhimu wa viongozi waliopo kutumia muda uliosalia kuitisha mkutano wa wanachama wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Geita (GEREMA), ili kufanya uchaguzi wa viongozi wapya.
Kwa upande wao, baadhi ya wanachama wa GEREMA, wakiwemo Misana Nyabange na Godfrey Miti, wameelezea hitaji la kuharakisha mchakato wa uchaguzi ili kuanza maandalizi ya uchaguzi katika ngazi za wilaya na matawi mengine ya wachimbaji wadogo.
Uchaguzi huu unatajwa kuwa muhimu kwa kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata wawakilishi ambao wataweza kutetea maslahi yao katika Mkutano Mkuu wa FEMATA na kusaidia kuendeleza sekta ya uchimbaji mdogo wa madini nchini.