Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wanachama na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM katika Ukumbi wa Kagwa, Lindi mjini.
Kabla ya mkutano huo wa ndani, Katibu Mkuu na msafara wake, walioko katika ziara mikoa ya Mtwara na Lindi, alipokelewa rasmi kwa kuvalishwa skafu na kufanya Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Lindi, katika Ofisi za CCM mkoani humo.
Katika ziara hiyo ambayo inalenga kukagua uhai wa chama,kusikiliza kero za wananchi,kukagua utekekezaji wa Ilani ya CCM,Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.







Comments
Post a Comment