Mbunge Ghati Chomete Afanikisha Upatikanaji wa Shilingi Milioni Sita Katika Uzinduzi wa Album ya Nimeelewa Somo
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete, Jana tarehe 14 Julai 2024 amefanikisha kupatikana kiasi cha shilingi milioni sita wakati wa uzinduzi wa Album Mpya ya "Nimelielewa Somo" Kanisa la TPC-Tarime.
Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Mara, amekuwa na mvuto mkubwa katika jamii hasa kutokana ushiriki wake mkubwa katika shughuli mbakimbali za jamii ndani na nje ya mkoani Mara,ikiwa ni pamoja na kuchangia Katika miradi mbali mbali ya maendeleo bila ya ubaguzi.
Katika hafla hiyo fupi Mhe. Ghati Chomete na marafiki zake wakichangia Takribani Millioni Tatu (Tsh.3,000,000/=) huku mbunge wa Tarime mjini Mhe.Michael Kembaki akichangia Fedha Taslimu Shillingi Millioni Moja (Tsh.1,000,000/=).
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Ghati ambaye alikuwa mgeni rasmi, amempongeza Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa jinsi serikali yake inavyoshirikiana na madhehebu ya dini kwa katika Shughuli mbakimbali za maendeleo yakiwemo ya kijamii na kiuchumi.


Comments
Post a Comment