Na Helena Magabe-Tarime
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara(BAWACHA) Mhe.Veronica Irecho ametoa Wito Kwa wanawake Mkoani Mara kujitojeza Kwa wingi kujiandisha Kupiga Kura pamoja na Kugombea Nafasi Mbalimbali za Uongozi na hivyo Kushiriki kikamilifu Katika shughuli za maendeleo.
Akizungumza katika kikao cha 7 tangu aanze ziara ya kuhamasisha uhai wa Bawacha Majimboni kilichofanyika katika ofisi ya chadema Tarime mjini Amesema lengo ni kuhamasisha wanawake kujiandikisha kupiga kura,kugombea nafasi mbali mbali sambamba na kukemea vitendo vya rushwa ndani ya Chama hicho
Ikiwa ni mara ya kwanza kukutana na Wajumbe wa Bawacha wa Tarime amekemea vikali vitendo vya rushwa ambapo amewataka wanawake kuepuka ushiriki Vitendo vya rushwa kwani ni mbaya na itapelekea kukosa nafasi mbali mbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 pamoja na Serikali kuu 2025.
Irecho ambaye ni Diwani Mstaafu wa viti maalumu pia amechangia mifuko 5 ya simenti kwa ajili ya ofisi ya chama na kusema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kina utaratibu wa kuchangishana na kujitolea na mambo yanenda sawa, lakini kwa sasa anasikitika kuona yale ambayo yalikuwa yakilalamikiwa kwenye baadhi ya vyama hasa rushwa kwa Sasa ndiyo yako Chadema, kwani wanachama wakiitwa kwenye vikao waanza kuhoji juu ya kulipwa posho na mengineyo ambayo hayafai kwenye chama chao.
" Chukueni fomu mjaze kwa hiyari mkishinda tumikieni Taifa acheni tamaa ni mbaya kemeeni rushwa aliyewavagaa taama huzaa dhambi jimboni kwangu pia kuna hiyo shida mtu akiitwa anaanza kuhoji atatupa nini atatulipa posho fanyeni kazi kama mlikuwa mmelala muamke vinginevyo mjiandae kuniona adui ntakuwa mkali" Amesema Irecho
Aidha amesema kikao kingine cha Jimbo la Tarime vijijini kitaketi hapo Julai 17 katika ofisi ya Tarime mjini huku akisisitiza wanawake kuwa mstari wa mbele kupinga rushwa ndani ya chama na kiahidi kutumia Wadau pamoja na wakufunzi kwenye Chama kuwapa semina wanawake hoja iliyotilewa na Mjumbe Prisca Hassan kuwa Wanawake wa chamema wapigwe msasa kujengewa uwezo.
Mwenyekiti wa Kanda Mhe Lucas Ngoto amesema Biblia inasema Wanawake ni Jeshi kubwa hivyo wasaidie Chadema kuingia madarakani sio kwa kugombea tu bali kwa kutoa maoni ni nani anafaa kugombea Serikali za mitaa na anayefaa kugombea Serikali kuu na wasikubali kiongozi yoyote kuwadanganya kuwapa viti maalumu huyo ni tapeli.
Amesema lazima chama kiweke utaratibu wa kutokomeza rushwa nakuwepo nidhamu kwani kukosekana maadili sio kwa Vijana pekee au wazee wapo kina mama ambao hawana breki juu ya kipi waongee hivyo ameonya vikali kuwa chama cha Chadema ni lazimiza kiwe na msingi imara wa maadili.
Kwa upande mwingine wamejitokeza watia nia watatu wa kugombea ubunge Jimbo la Tarime mjini ambao ni Esther Nyabulili, Ferista Joseph Marigo pamoja na Rejina Mbusha ambaye ni Mjumbe wa Bawacha Mkoa na Mc maarufu Tarime mjini pamoja na Zakayo Wangwe ambaye ni mwanasheria amewatia moyo kina Mama Wajane waliopoteza waume zao hifadhini na mgodini,




Comments
Post a Comment