Na Angela Sebastian-Bukoba
Naibu waziri wa maji mhandisi Kundo Mathew amewaagiza waandisi wa mamlaka za maji nchini kukamilisha miradi iliyokwama pasipo kuanzisha miradi mipya
Mhandisi Mathew amesema hayo alipowasili katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa ziara ya siku tatu na kupokea taarifa ya kaimu mkuu wa mkoa wa Kagera Erasto Sima aliyeomba serikali kusaidia wananchi wa wilaya ya Bukoba kukamilishiwa mradi wa maji Kemondo ambayo umekwama kwa muda mrefu
Amesema kuwa lengo la Serikali ni kutaka kuahakikisha miradi ya maji ambayo imekwama inakamilika ili kuwaondolea wananchi adha ya upatikanaji wa maji safi hivyo waandisi wa mamlaka za maji nchini wanatakiwa kutekeleza agizo hilo haraka iwezekanavyo kwa maslai mapana ya wananchi.
"Hakuna sababu ya kutangaza miradi mingine wakati unao mradi uliofikia asilimia 70 au 80 ukauwezesha kukamilika lakini pia hatutaki tuwe na mchakato mrefu wa manunuzi kwasababu sheri imerekebishwa sisi Wizara na Ruwasa makao makuu tunatoa vibali hivyo Mhandisi atakayepata kibali akakaa nacho hatutoelewana"ameagiza Kundo.
Awali akitoa taarifa ya mkoa, mkuu wa wilaya ya Bukoba ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Kagera amesema kuwa licha ya uwepo wa miradi ambayo imekwama muda mrefu ikiwemo mradi wa kemondo maeneo mengine yapo safi wananchi wamkoa wa Kagera wanapata maji safi na salama.
Amepongeza ushirikiano walionao kati ya waandisi wa mamlaka za maji wa RUWASA na BUWASA wa mkoa wa Kagera kwa jinsi wanavyotekeleza majukumu yao kwa maslai ya wananchi wa mkoa wa Kagera.
Aidha akiwa katika ofisi za chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa huu alipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kutoka kwa katibu wa Christopher Pallangyo ambaye amesema upo mradi wa kemondo na Buhembe ambayo imekwama hivyo ikamilishwe ili kufikia lengo la Serikali.

Comments
Post a Comment