Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Ndugu Stephen Wasira, amefungua rasmi mafunzo kwa vyama sita rafiki vya ukombozi kutoka kusini mwa Afrika. Mafunzo hayo yamefanyika leo, Mei 18, 2025, katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Leadership School, Kibaha Mkoa wa Pwani
Vyama vinavyoshiriki ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ZANU-PF, African National Congress (ANC), SWAPO, FRELIMO, na MPLA.
Mafunzo haya yanalenga kuwajengea makada kutoka vyama hivyo sita uwezo wa kiuongozi, usimamizi, na kuendeleza tunu za harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.











Comments
Post a Comment