Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, akisalimiana na viongozi Mbalimbali Mara baada ya kuwasili Bungeni leo Mei 19, 2026 kwa ajili ya kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2026/27.
Wasilisho hilo linatarajiwa kueleza vipaumbele vya wizara, utekelezaji wa shughuli mbalimbali za ulinzi na usalama pamoja na mipango ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2026/2027
Viongozi ambao anasalimiana nao pichani ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Faraji Kasidi Mnyepe
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob Mkunda pamoja na viongozi wengine waandamizi.






Comments
Post a Comment