Tanzania Yaendelea Kung’ara Duniani Katika Sekta ya Utalii, Yashika Nafasi ya 6 Afrika na Mashariki ya Kati
TANZANIA imeendelea kufanya vizuri katika sekta ya utalii duniani, ambapo imefanikiwa kushika nafasi ya 6 katika ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati kwa ukuaji wa watalii wa kimataifa, huku pia ikiorodheshwa nafasi ya tatu duniani kwa masoko ya utalii yaliyofanya vizuri zaidi kwa matumizi ya watalii mwaka 2025 ukilinganisha na mwaka 2024.
Akieleza mafanikio hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema hatua hiyo ni uthibitisho wa mafanikio ya sera na mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kukuza sekta ya utalii nchini.
Amefafanua kuwa mafanikio hayo yametokana na maboresho ya miundombinu ya utalii, uimarishaji wa vivutio vya asili, kuimarika kwa huduma kwa wageni, pamoja na kampeni za kimkakati za kuitangaza Tanzania katika masoko ya kimataifa.
Waziri Kijaji amesisitiza kuwa mwitikio mkubwa wa watalii na ongezeko la matumizi yao nchini ni ishara ya kuimarika kwa ushindani wa Tanzania kimataifa, hatua inayochangia kwa kiasi kikubwa kukuza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.









Comments
Post a Comment