Katambi-Serikali yaokoa Bilioni 21 Magereza

GEORGE MARATO TV
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema jumla ya Shilingi Bilioni 21 zimeokolewa ikiwa ni faida za Bodi ya Parole na Programu ya Huduma kwa Jamii.

Ametoa kauli hiyo katika Viwanja vya Jeshi la Magereza wakati  Hafla ya Kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi Namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi Namba 48 kwa mwaka 2025/2026 iliyohitimishwa na Mgeni Rasmi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Ukonga jijini Dar es Salaam.

“Tumeanza kutekeleza maelekezo yako ya Tume ya Haki Jinai ambayo wewe Mheshimiwa Rais uliiunda ili kuweza kufanya Maboresho kwa kuzingatia haki za binadamu na kuhakikisha wafungwa ambao ni wanafunzi wetu wa maadili wanapata na kutendewa haki stahiki za kibinadamu ikiwemo pia mahakama inayotembea ili kuweza kutoa hukumu kwa wakati na Mheshimiwa Rais watanzania wanakushukuru kwa kuweza kutoa msamaha kwa wafungwa 1369 ambapo umetumia kifungu cha 45 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hatua hiyo imetusaidia katika kupunguza gharama na kupunguza msongamano magerezani.” amesema Waziri Katambi 




Waziri Katambi pia amezungumzia maelekezo ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo Kamati ya Parole na Huduma za Programu ya Huduma kwa Jamii zimefanya kazi ambapo jumla ya wafungwa 5000 wanatumikia vifungo vya nje huku akiweka wazi gharama za chakula,mahitaji ya maji na umeme zingeharimu serikali Shilingi Bilioni 21 .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top