WAZIRI wa Maji, Juma Aweso, amesema Serikali inaendelea kupiga hatua katika upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, ikilenga kufikia asilimia 90 vijijini na asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2030.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni leo Mei 5, 2026, Aweso alisema hadi Desemba 2025, huduma ya maji vijijini imefikia asilimia 85.2 kutoka asilimia 83.1 mwaka 2024. Mafanikio hayo yametokana na kukamilika kwa miradi 54 yenye vituo 946 vya kuchotea maji, vilivyonufaisha wananchi zaidi ya 493,932 katika vijiji 151.
Kwa mujibu wa Aweso, Amesema hatua hiyo imeongeza idadi ya wananchi wa vijijini wanaopata huduma ya maji kufikia zaidi ya milioni 38.6.
Kwa upande wa mijini, upatikanaji wa maji umefikia asilimia 92.5 hadi Desemba 2025, ukiongezeka kutoka asilimia 90.6 mwaka uliopita.
"Hali hii imechangiwa na kukamilika kwa miradi 12 inayohudumia watu 880,633, huku miradi mingine 214 ikiendelea kutekelezwa". Amesema
Kuhusu usafi wa mazingira, Waziri Aweso amesema juhudi za Serikali zimeleta mafanikio makubwa hasa vijijini, ambapo matumizi ya vyoo bora yamefikia asilimia 98.9 kupitia kampeni za kitaifa za uhamasishaji na elimu kwa umma.
Ameongeza kuwa mijini, huduma za majitaka zimeboreshwa kupitia upanuzi wa mitandao, ujenzi wa mitambo ya kutibu majitaka na udhibiti wa umwagaji holela, hatua zinazolenga kulinda vyanzo vya maji na kuboresha mazingira ya makazi.





Comments
Post a Comment