Mawaziri Wajadili Udhibiti wa Silaha na Usalama wa Kikanda

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobass Katambi, ameshiriki mkutano kwa njia ya mtandao wa Kamati Ndogo ya Mawaziri ya Kikanda ya Udhibiti wa Silaha ndogo na nyepesi katika Ukanda wa Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika (RESCA).

Mkutano huo umewakutanisha mawaziri wa usalama kutoka nchi wanachama, ukilenga kujadili hali ya usalama katika ukanda huo pamoja na changamoto zinazoendelea kujitokeza, hususan usambazaji na matumizi haramu ya silaha ndogo na nyepesi.

Nchi zilizoshiriki mkutano huo ni pamoja na Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Rwanda, Uganda, Kenya, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Ethiopia, Eritrea na Djibouti, ambapo zimejadili kwa pamoja masuala ya udhibiti wa silaha na mapambano dhidi ya biashara haramu ya silaha.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri Katambi amesema serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imejipanga kimkakati kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuboresha mifumo ya udhibiti wa uingizaji silaha nchini.

Ameeleza kuwa hatua hizo zitajumuisha kuangalia kwa kina dhana ya umiliki na wajibu wa mmiliki wa silaha, tathmini ya matumizi sahihi ya silaha, ukaguzi wa silaha, pamoja na kuchunguza lengo na dhamira ya waombaji na wamiliki wa silaha.

Aidha, amesema serikali itaimarisha pia mifumo ya kiteknolojia na kidijitali katika kudhibiti silaha ili kuhakikisha usalama unadumishwa katika ukanda huo na nchi kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top