Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Aprili 7, 2026, amehani msiba wa Mstahiki Meya Mstaafu wa Jiji la Zanzibar, Marehemu Mahmoud Muhammed Mussa, nyumbani kwa marehemu Zanzibar.
Marehemu Mahmoud Muhammed Mussa alifariki Aprili 6, 2026. Wakati wa uhai wake, aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali, ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi (BLW).






