Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya China zimepanga kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kuzuia Uhalifu ikiwemo mashirikiano katika Sekta ya Uchunguzi wa Uhalifu,Uhalifu wa Kimtandao(Cyber Crime)na suala nzima la kubadilishana watuhumiwa wa uhalifu baina ya Nchi hizo mbili.
Hayo yamebainika wakati wa Kikao Kazi Kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi na Balozi wa China nchini Tanzania,Chen Mingjian ambapo pia waliweka wazi mashirikiano hayo pia kuhusisha ubadilishanaji wa teknolojia mbalimbali za Kudhibiti Uhalifu katika maeneo muhimu.
Kikao hicho kimefanyika Ofisi Ndogo ya waziri,jijini Dar es Salaam.






