MwanaFA, Kingwendu wafanya mazungumzo ya kimkakati kuhusu sanaa

GEORGE MARATO TV
0


Na Mashaka Mhando

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amekutana na kufanya mazungumzo na msanii mkongwe wa vichekesho nchini, Kingwendu, yaliyolenga kujadili fursa za kimaendeleo katika sekta ya sanaa.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Mwinjuma amesema Wizara imejizatiti katika kuimarisha mazingira yatakayowawezesha wasanii, hususan wakongwe, kunufaika na kazi zao kupitia mifumo rasmi ya kibiashara.

Amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa wasanii wakongwe katika kujenga tasnia ya sanaa na vichekesho nchini, hivyo kuna haja ya kuoanisha uzoefu wao na fursa mpya zinazojitokeza katika soko la sasa la kidijitali.

“Tumekutana na Kingwendu kujadili namna wasanii wetu wanavyoweza kutumia fursa mbalimbali za kimaendeleo zinazojitokeza hivi sasa ili kusaidia ukuaji wa sekta ya sanaa na mnyororo mzima wa thamani,” amesema Mwinjuma.

Kwa upande wake, msanii Kingwendu amepongeza hatua ya Wizara kuwa karibu na wadau wa sanaa, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kutatua changamoto zinazowakabili wasanii nchini na kuongeza kasi ya ukuaji wa tasnia hiyo.



Kikao hicho ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya Naibu Waziri Mwinjuma na wadau wa sekta za habari, sanaa na michezo inayolenga kukusanya maoni na kuboresha sera za uwezeshaji wasanii nchini. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top