Mhe Esther Matiko Ashiriki Mazishi ya Frank Peter Zakaria Mjini Tarime

GEORGE MARATO TV
0


Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther Matiko ameshiriki mazishi ya Frank Peter Zakaria mtoto wa Chief Peter Zakaria mjini Tarime.

Akizungumza na waombolezaji wa msiba huo, Mhe Esther Matiko ametoa salamu za pole na rambirambi kwa familia ya Chief Peter Zakaria kwa kuondokewa na kijana wao mpendwa.




Sambamba na salamu hizo za pole Mhe Esther Matiko ameyaelezea mahusiano chanya ya Frank na wananchi wa Tarime, Nyamongo, Mwanza na kwingineko alikopata kuishi siku za uhai wake.

“Leo hii tumekusanyika hapa kwa wingi kuomboleza kifo cha Frank umati huu wote ni kwa sababu ya mahusiano chanya Chief Peter Zakaria kwa wananchi wa Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla. Kata ya Turwa hatukuwa na eneo la kujenga kituo cha afya lakini Chief Peter Zakaria ametupatia eneo zaidi ya hekali 4 bure kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya” amesema Mhe Esther Matiko

Akihitimisha salamu za pole na rambirambi kwa wafiwa na waombolezaji Mhe Esther Matiko amewashukuru Wananchi wa Tarime mjini na waombolezaji wote jinsi  wanavyoshirikiana kwenye shida na raha kama ndani ya mji wa Tarime na nje ya Tarime.

*Bwana Alitoa Bwana Ametwaa*

*Jina la Bwana lihimidiwe.*

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top