Waziri Mkuu Aweka Jiwe la Msingi Shule ya Sekondari Mgombe Yenye Mkondo wa Amali ya Kihandisi, Katavi

GEORGE MARATO TV
0


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 15, 2026 ameweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari Mgombe yenye mkondo wa Amali ya Kihandisi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo.


Ujenzi wa shule hiyo unatekelezwa kupitia Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 1.694 na hadi sasa umefikia asilimia 99 ya utekelezaji.

Shule hiyo itatoa mafunzo ya amali katika fani mbalimbali zikiwemo ufundi magari, ufundi bomba, mifumo ya umeme wa jua pamoja na ufundi umeme wa magari. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo utakaowawezesha kujiajiri, kuajiriwa au kuendelea na masomo ya elimu ya juu.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top