Mabadiliko Makubwa Yaja Wizara ya Mambo ya Ndani_Katambi

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na Uboreshaji wa Ofisi, Makazi, Vifaa vya Kazi, Maslahi, Mikakati na Mafunzo ili vyombo hivyo viweze kujitegemea ambapo pia amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Ofisi za Mji wa Serikali,Mtumba.

Ametoa kauli hiyo wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Gereza la Msalato jijini Dodoma ambapo mradi huo unajengwa wa wakandarasi wa ndani ya Jeshi la Magereza huku wafungwa wakipata fursa ya kushiriki ujenzi huo ikiwa ni mpango wa kuwawezesha kupata ujuzi sambamba na utekelezaji wa dhana ya urekebu kwa wafungwa hao ili wakimaliza vifungo wawe na ujuzi waliopata wakati wakitumikia vifungo.






Akizungumza katika ziara hiyo,Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,CGP Jeremiah Katungu amesema gereza hilo kukamilika kwake litaweza kuhifadhi wafungwa 1080 ambapo pia linajumuisha kituo cha afya,chumba cha mahakama mtandao ambacho kitasaidia baadhi ya kesi kuendeshwa bila mtuhumiwa kwenda mahakamani ikiwa ni uboreshaji wa uendeshaji wa kesi kwa kutumia teknolojia.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top