Twcc Mara Wapongeza Mfumo Jumuishi wa TRA Kwa Kuokoa Muda Kwa Wafanyabiashara Nchini.

GEORGE MARATO TV
0


Na Mwandishi wetu Jovina Massano.

Katibu wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania TWCC Mkoa Wa Mara Anastazia Maximilian ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuiboresha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuweka mfumo bora wa huduma za mapato hapa nchini.

Akizungumza mwandishi wetu katibu huyo amesema mpango wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wa kuja na Mfumo Jumuishi wa Utawala wa Mapato ya Ndani(IDRAS) utawezesha kuokoa muda kwa wafanyabiashara sambamba na kuondoa usumbufu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiwemo kupunguza ghalama kwa walipa Kodi.

"Mfumo huu unamanufaa makubwa kwetu sisi wafanyabiashara kwa kuwa umetuondolea adha ya kutembea na nyaraka wakati wa kuwasilisha ritani na kulipia Mapato hii inatusaidia kuepuka upotevu wa nyaraka lakini pia utatuwezesha kujihudumia mwenyewe kupitia mfumo huo wa IDRAS"amesema Anastazia.

Aidha ameipongeza TRA kwa kutambua thamani ya lugha ya Kiswahili kwa kuwezesha kuwa mojawapo ya lugha zinazotumika katika Mfumo wa IDRAS ambapo inasaidia kwa wasiojua lugha ya kiingereza kutumia bila tatizo lolote.

Ameongeza kuwa umakini wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan umewezesha kuboresha  mifumo ya utoaji huduma inayokwenda kwa wakati inayoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani.

Hakusita kuwahimiza wafanyabiashara ambao hawakupata fursa ya kupata elimu ya namna ya kutumia mfumo jumuishi wa IDRAS kufika ofisi za TRA kuweza kupata uelewa kuondokana na usumbufu katika biashara zao.

Nae mfanyabiashaAloyce Masatu Lawi wa Mtakuja A Kata ya Mwisenge amesema mfumo huo ni mzuri Serikali imefanikiwa kuendana na mabadiliko ya kidunia hii inaonyesha dhahiri uwajibikaji kwa wafanyabiashara kwa kujali muda katika kukuza uchumi wa watu na nchi kuleta maendeleo nchini.

"Niiombe Mamlaka ya Mapato Tanzania uendelee kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili hata wasioweza kutumia  wenye simu za kawaida hasa walio vijijini na pembezoni waweze kunufaika na huduma hiyo", amesema Aloyce.

Januari 30,2026 TRA mkoa wa Mara walihitimisha zoezi la uelimishaji ndani ya Manispaa ya Musoma katika ukumbi wa MK uliopo Kata ya Mwisenge.


Ambapo meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA)mkoani hapa Nasoro Ndemo amewashukuru wafanyabiashara kwa kuwa na ari  kujitokeza kwa wingi kupata uelewa wa Mfumo Jumuishi ambao utaleta tija kwa wafanyabiashara .

Ikumbukwe kuwa Mfumo huu wa IDRAS umeanza kufanya kazi Februari 9,2026 ukiwa na lengo la kuondoa kukutana zaidi baina ya afisa wa TRA na mfanyabiashara na kuifanya mifumo izungumze na kuondoa malalamiko katika malipo ya kodi kwa kuwa mfanyabiashara ataona taratibu na Sheria za kodi na kulipa kiwango anachostahili kulingana na shughuli husika.

Elimu ya mfumo itakuwa endelevu ili kuwafanya wananchi kujua haki na wajibu wao na watajua sheria na umuhimu wa kodi katika Taifa. 

"Kila Wilaya kutakuwa na madawati maalum ya uelimishaji ambapo afisa ambae atakuwa anatatua na anawasikiliza wafanyabiashara wanaoshindwa kutumia mfumo wa IDRAS na kuwaelimisha kwa ufasaha na kutatua changamoto zinazokuwa zimejitokeza,"amesema Nasoro.

Kwa Upande wake afisa msimamizi wa kodi  Rebeca Hezron  amesema Mfumo huu umekuja na mapinduzi makubwa ya kiteknolojia ambapo huduma zote za TRA zinapatikana kupitia mtandao kutakuwa hakuna haja ya mhitaji kufunga safari kufika ofisi za Mamlaka ya mapato.

"Mfumo huu umezingatia lugha zote na unatoa huduma siku saba za wiki masaa 24 kuanzia kujisajili, mrejesho wa kodi mpaka kwenye kuandika barua ikiwemo kutuma ritani za kodi bila kufika ofisi za Mamlaka ya mapato",amesema Rebeca.

Maboresho haya yanawezesha kuokoa muda ghalama na usumbufu kwa wafanyabiashara hasa wanaokuwa mbali na ofisi za Mamlaka lakini Mamlaka pia ijitahidi kuhakikisha Mfumo huu unatoa huduma kwa kasi kwa wateja pasipo usumbufu.

Imani kwa wafanyabiashara kwa ujio wa Mfumo huu Mamlaka tayari imefanya tathmini kwa wahitaji wake na kuhakikisha kuwa huduma ya mtandao inakuwa haina usumbufu kwa wafanyabiashara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top