Vijiji Vinane Misungwi Kunufaika na Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi

GEORGE MARATO TV
0


 Wananchi waupokea kwa furaha Mpango wa kitaifa wa matumizi bora ya Ardhi unaotekelezwa katika Vijiji 8 vya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza .

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, na Maendeleo ya Makazi pamoja na Timu ya Wawezeshaji wa masuala ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi bora ya Ardhi mapema wiki hii imetambulisha mpango huo wa matumzi bora Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi utakaotekelezwa katika Vijiji 8 kati ya Vijiji 115 vya Wilaya hiyo kwa kutenga maeneo rasmi kisheria kwa matumizi ya huduma za kijamii sambamba na kutoa hati za kimila.

Akizungumza katika Mikutano ya Hadhara na Viongozi wa Serikali za Vijiji katika Kijiji cha Gulumungu na Lukanga Afisa wa Tume ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bw. Bwahama Bagenyi ameeleza kwamba Serikali inaendelea kuboresha na kuweka mipango ya upimaji wa maeneo ya Vijiji kwa ushirikiano na Wananchi pamoja na Viongozi, waweze kutenga maeneo yao kwa ajili makazi, Kilimo, malisho, Makaburi, taasisi za umma, na maeneo ya hifadhi ya misitu na huduma za kijamii.



Aliongeza kwamba zimeundwa Kamati mbalimbali ikiwemo Kamati ya usimamizi wa Ardhi, Kamati ya uhakiki wa Mipaka na Baraza la Ardhi la Kijiji ambazo zitahusika katika usimamizi na ufuatiliaji wa maeneo na kutatua na kusuluhisha migogoro midogo midogo ya Ardhi, na lengo kubwa ni kukuza thamani ya ardhi na Wananchi waweze kupewa hati miliki za kimila.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama amesema kwamba ameupokea Mpango huo wa Matumzi bora ya Ardhi ambao unaendelea kutekelezwa katika Vijiji vya Wilaya hiyo na umelenga kuboresha mazingira na kukuza uchumi wa Wananchi wote sambamba na kuleta maendeleo ya kiuchmi na kijamii na kuwasihi Wataalam wa Ardhi kutekeleza kikamilifu na kwa weledi.

Ameeleza kuridhishwa na hatua za makusudi za Serikali katika kuendelea kupanga na kupima Ardhi katika Vijiji ili Wananchi waweze kunufaika kwa kujiongezea kipato na kupata maendeleo hatimaye kuinua uchumi katika Wilaya na tifa kwa ujumla.

Kwa upande wao baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Lukanga na Gulumungu wameonyesha na kueleza furaha yao kwa kuupokea mpango huo akiwemo Bi. Elizabeth Joseph Kaniki ameeleza kwamba kwa sasa akina mama wataweza kumiliki ardhi bila wasiwasi pamoja na Bw. Herman Machuma amesema mpango huo umeleta faida na manufaa makubwa, migogoro itapungua baina ya Wafugaji na Wakulima kutokana na uwepo wa maeneo ya malisho na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Kilimo na huduma za kijamii.

































Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top