Akizungumza katika kikao hicho, Kanali Mtambi amewataka vijana wa Wilaya ya Tarime kubadilika kifikra na matendo ili kuweza kufaidi fursa mbalimbali zilizopo katika Wilaya ya Tarime na Mkoa wa Mara kwa jumla.
Mhe. Mtambi amesema Mji wa Tarime na Mkoa wa Mara unafursa nyingi na kusipokuwa na amani na utulivu fursa hizo zitawafaidisha watu waliopo katika Mikoa mingine.
Mhe. Mtambi pia amewasikiliza vijana na kupokea kero, changamoto na mapendekezo yao kuhusiana na utatuzi wa changamoto zinazowakabili.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Chifu wa Watimbaru Ndugu Peter Zakaria na viongozi wengine katika jamii na kimefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya CMG, Tarime.














