Mwanafa Akutana na Baraza la Madiwani Muheza

GEORGE MARATO TV
0


📍Awataka wahamasishe mapato katika kata zao, waiongezee uwezo halmashauri

*Na: Mwandishi wetu, Muheza*

MBUNGE wa Jimbo la Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), amefanya kikao kizito na madiwani wote wa wilaya hiyo leo, akisisitiza umuhimu wa **umoja, uwazi na utekelezaji wa haraka** wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na baraza hilo jipya la madiwani, Mhe. MwanaFA aliwapongeza kwa ushindi mnono wa Oktoba 29 na kuwataka sasa kusahau yaliyopita na kuungana pamoja kuleta maendeleo Muheza.

> “Ushindi huu unatakiwa sasa tuongeze ushirikiano na umoja, na **tuvunje makundi** kwa sababu sasa Muheza ni Moja,” Mhe. MwanaFA alisisitiza, akiongeza kuwa yeye atashirikiana na madiwani wote bila kubagua.


*KUHAMASISHA MAPATO YA HALMASHAURI**

Mbunge huyo aliwakumbusha madiwani kuhusu umuhimu wa kuhimiza watendaji wakusanye mapato ili halmashauri iweze kupata uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa miradi ya Halmashauri.

Alisema halmashauri inapoongeza mapato ya ndani (Own Source) inaweza kusaidia miradi ya maendeleo katika kata hivyo akawataka waisimamie halmashauri iweze kutimiza malengo yake ya ukusanyaji wa mapato.

Lakini pia aliwaagiza madiwani kukaa na Watendaji wao wa Kata na kutengeneza **Mpango Mkakati wa maendeleo wa miaka mitano ijayo** ndani ya **siku kumi** zijazo, ili yeye kama Mbunge aweze kuisukuma mbele serikalini.


Mhe. MwanaFA pia alisisitiza:

* **Mahusiano na Wananchi:** Madiwani wanapaswa kushiriki shughuli za kijamii na kukaa na wananchi mara kwa mara.

* *Kasi ya Maendeleo:* Kuwakumbusha wananchi kazi nzuri iliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan huku wakiongeza kasi ya maendeleo.


*AHADI NA SHUKRANI*

Akizungumzia uteuzi wake mpya, Mhe. MwanaFA alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini tena, akiahidi **hata muuangusha** katika nafasi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, nafasi aliyokuwa nayo Baraza lililopita.

Awali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza, Salimu Shechambo, aliwashukuru madiwani kwa kumpa wadhifa huo na kuahidi kushirikiana nao katika kazi za kuijenga Muheza mpya huku akienda na kauli mbiu ya *Umoja na Ushirikiano* katika kipindi chote cha miaka mitano.

Diwani wa Kata ya Kicheba, Hamis Mkodingo, alitumia fursa hiyo kumkumbusha Mbunge kufuatilia ujenzi wa *barabara ya Afrika Mashariki* inayopita maeneo muhimu, ambapo Mbunge alitaka suala hilo liwekwe kwenye taarifa rasmi za mpango kazi wa kata kwa ajili ya ufuatiliaji wa kina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top