Serikali yatangaza mipango mikubwa sekta ya elimu

GEORGE MARATO TV
0

 

Waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia, Mh. Profesa Adolf Mkenda amesema serikali imejipanga kuanzisha mfumo wa elimu ya lazima ya miaka 10 ifikapo mwaka 2028 ili kuongeza ubora wa taaluma ya elimu nchini.


Akizungumza mapema hii leo Disemba 10, 2025,  Profesa Mkenda katika Mkutano wa mawaziri na waandishi wa habari uliyoandaliwa na idara ya habari maelezo katika ofisi ya kituo cha ukombozi jijini dar es salaam ambapo pia amesema ustawi wa sekta ya elimu chini ya serikali ya Rais Samia umekua kwa zaidi ya asilimia 75 ambapo wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wamefanikiwa kwenda sekondari.

Aidha, amesema kuwa serikali imejipanga kuongeza masomo ya lazima ya biashara na kiingereza ili kuweza kusaidia wanafunzi wenye ndoto za kibiashara kuweza kufundishwa mbinu mbalimbali na hatua muhimu za kibiashara ili kuwasaidia wenye ndoto za ufanyaji biashara.



Pia, Waziri Mkenda amesema katika kutambua umuhimu wa elimu ya amali nchini serikali imejipanga kutoa elimu ya ufundi katika kidato cha nne  hali itakayomsaidia mwanafunzi kutunukiwa cheti cha ufundi kitakachoweza kumsaidia kwenda kujitegemea kwa kupata ajira au kujiajili.

Katika hatua nyingine serikali imeanzisha programu ya Samia schoolarship ili kuweza kusaidia wanafunzi nchini katika nyanja ya teknolojia ambapo matarajio ni kusafirisha wanafunzi 50  kwenda kujifunza katika mataifa ya nje ili kuweza kuwaongezea uzoefu wa kitaaluma vijana wa kitanzania.

Kufuatia kuongezeka kwa waandaaji wa maudhui ya kimtandao nchini serikali imejipanga kwaandaa kitaaluma waandaaji hao ili kuweza kufanikisha kuwajengea uwezo ili kuwezeaha wafikie malengo yao.




Hata hivyo Waziri Mkenda amesema kuwa serikali ina mpango wa ujenzi wa shule ya michezo hali itakayosaidia kuhamasisha vijana mashuleni kuendelea na shule kwani baadhi ya wanafunzi wamekuwa na wakati mgumu wa kutoendelea na shule kwa sababu ya kukosa michezo mashule hali inayopelekea kukatiza masomo katika shule mbalimbali nchini.

Pia, Waziri Mkenda amesema serikali inatambua uwepo wa idadi ya wanafunzi kuishia kati masomo hivyo imejipanga kuja na mfumo utakao wezeaha kuwafuatilia wanafunzi ili kuweza kutambua sababu ya kukatiza masomo yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top