Dkt.Mwigulu afunga semina elekezi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri

GEORGE MARATO TV
0


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 04, 2025 amefunga semina elekezi kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.


Semina hiyo ambayo ilifunguliwa na Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ilikuwa na lengo la kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu majukumu, taratibu, maadili na matarajio ya Serikali kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla. 



Akizungumza katika semina iliyoandaliwa kwa ajili ya Baraza la Mawaziri, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa maarifa waliyoyapata yatasaidia kuwaongoza katika kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, Rasilimali za Umma, Dira 2050, Mipango ya Maendeleo na kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top