KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Asha Rose Migiro amesema Watanzania wote kwa pamoja, wanaowajibu wa kuhakikisha taifa linakuwa salama kwa misingi na mazingira mazuri ya kusonga mbele.
Akizungumza leo Alhamis tarehe 4 Desemba 2025, jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Jukwaa la Wanawake ambao wamekutana na mazungumzo kati ya Tanzania, wakitumia kauli mbiu inayosema “Mama ni Amani.”
"Tumekutana kama kina mama na kauli mbiu yetu inatuambia mama ni amani. Anapokuwepo mama kuna amani kwa namna mbalimbali. Nitumie nafasi hii kuleta salamu kwenu kutoka kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
“Anajua kina mama tunakutana leo, anajua kina baba wataungana nasi leo, anajua vijana wake pamoja na taifa hili zinaonesha vijana ni sehemu kubwa sana ya Taifa letu.
“Kwa hiyo Rais Samia anatoa salamu za pekee kwenu na amefurahi kusikia vijana kuungana mama zenu, baba zenu na walezi wenu katika mada hii muhimu ya mama ni amani,” amesema Balozi Dkt. Migiro.
Balozi Migiro alisema pia kuwa hatua hiyo inakwenda sambamba na falsafa ya Rais Samia ya mambo manne, ambapo mmoja mmoja ni ustahimilivu. Akisema kuwa, pamoja na changamoto zilizojitokeza, bado nchi yetu imesimama imara.
“Na kupitia yale ambayo tumeona na Rais ameyaeleza nchi yetu iko tayari kujenga upya, nchi iko tayari kuimarisha mazuri na ndio maana jukwaa leo limewaleta wanawake na vijana kwa sababu Tanzania ni yetu sote.
"Sisi wote hatuna pakwenda ila hapa Tanzania kwa mantiki hiyo ujumuishi huu unahakikisha haturudi nyuma. Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ni mwanamke namba moja, ni kiongozi ni mama, ni mlezi. Leo tunapokaa hapa tunazungunza mchango wa amani katika ujenzi wa Taifa letu."
Aidha Katibu Mkuu CCM huyo alisisitiza umuhimu wa kwa ajili ya maridhiano, kwa ajili ya kwamba huu ni wakati wa Watanzania, wakiwemo wanawake, kuitikia mwito huo kwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya mazungumzo mbalimbali, ikiwa ni kujadili kiini cha vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu.
#Mwisho








