Vita,Vurugu Havijawahi Saidia Nchi yoyote-Simbachawene

GEORGE MARATO TV
0




Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amewataka wanaharakati na vijana kutafuta njia sahihi ya kudai haki na sio kutumia njia ambazo zinahatarisha usalama wa nchi ambao baaadhi ya nchi amani ilipotea na kupelekea kuzalisha wakimbizi ambao wameenea sehemu mbalimbali duniani ambapo pia amewahakikishia wananchi wa Tanzania amani na usalama kuelekea mwisho wa mwaka.

Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Pili unaohusisha Pande Tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani UNHCR ambapo pia walitumia mkutano huo kusaini nyaraka zinazoelezea Mpango wa Urejeshwaji wa Wakimbizi Elfu Themanini na Sita na Mia Mbili Hamsini na Sita kutoka nchi ya Congo.

‘Nchi yetu iko na amani na tunakokwenda katika Sikukuu za Mwisho wa Mwaka niwatakie Watanzania wenzangu sikukuu njema na wasiwe na hofu na tunapozungumza mambo haya ya kuwaambia wenzetu warudi kwao na sisi huku hatuna nafasi ya kuwahifadhi basi ni vizuri na sisi watanzania tukajifunza somo hili kwamba tuna wajibu wa kutunza amani yetu ili na sisi kesho tusije kugeuka wakimbizi…,’ alisema Waziri Simbachawene

‘….kwa hiyo vijana na wale wote wanaharakati ambao wanafikiri njia ya vurugu na fujo na kuvunja amani ndio itakayowapa haki yao hiyo njia ni ndefu mno,tunazungumzia Congo iliyovurugika miaka thelathini iliyopita amani yao aijarudi mpaka leo sasa wewe unaefikiria kuivuruga nchi yako ya Tanzania leo utakaa miaka thelathini nak ama wewe ni kijana basi hiyo haki utoiyona kwasababu umeidai kwa mfumo ambao sio rasmi,tuna mfumo rasmi wa mazungumzo,kuweka hoja mezani lakini vurugu haijawahi kuisadia nchi yoyote ndugu zetu wa Congo tunao hapa wanaitafuta hiyo amani iliyopotea kwa miaka zaidi ya thelathini.Sisi watanzania tuienzi amani yetu,tuilinde amani yetu hususani vijana kwani ikipotea amtoiona ikirejea,muwe wavumilivu.’ Alisisitiza Waziri Simbachawene.




Jumla ya Wakimbizi 238,956 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanahifadhiwa hapa nchini huku kutoka Burundi wakiwa 152,019 na mataifa mengine yakichangia idadi ya 681.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top