>Ameahidi kusimamia rasilimali za nchi
>Kuheshimisha utu na thamani ya mwanamke.
>Kuboresha Mishahara kuongeza ufanisi wa uwajibikaji.
>Kurudisha ujamaa
>Kufuata ndoto na nyayo za Rais wa awamu ya tano.
Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Democratic (DP) Abdul Juma Mluya amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atasimamia rasilimali zilizopo kunufaisha wazawa na kuondoa kikokotoo kwa watumishi wa serikali.
Ameyasema hayo Septemba 30 akiwa ziarani mkoani Mara wakati akinadi sera zake na kuwaomba wananchi wa mkoa huu kumchagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema huduma zinazotolewa hazikidhi haja za wananchi wa Tanzania kutokana na uwajibikaji mbovu wa viongozi kwa kuhujumu fedha za Umma.
Amesema endapo wananchi watamchagua hakutakuwa na tozo za janjajanja ataboresha huduma za Afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kutosha katika vituo vya afya nchini kote, huduma bora kwa akina mama wanakwenda kujifungua,wazee, watoto na watu wenye mahitaji maalum kwa kuondoa ghalama za matibabu.
Amesisitiza kuwa sio bure kwa sera na sheria halafu haitekelezeki itakuwa bure ili kuheshimisha utu , serikali ya DP itawajibika kutoa huduma ya lishe kwa mama atakaejifungua kwa muda wa miezi mitatu aweze kupata nguvu ya kumlea mtoto wake.
Ameahidi kuboresha mishahara kwa watumishi wa Umma wakiwemo walimu wauguzi na majeshi yote lengo ni kuongeza ufanisi na weledi kwa watumishi ili huduma za zipatikane kwa usawa.
Mishahara ikiboreshwa kwa watumishi wa Umma watakuwa na morali ya kuwatumikia wananchi kwa kuwa Mazingira ya kazi ni rafiki na kufanya kazi kwa starehe na yatapelekea kuondoa malalamiko kwa wananchi.
Upande wa elimu DP itaondoa michango kwa wanafunzi na kutengeneza mazingira mazuri kwa walimu ili waweze kufundisha kwa ufasaha.
"Siku hizi wanafunzi wanaacha shule shuleni wanarudi na makaratasi nyumbani hii ni kutokana na mazingira duni kwa walimu hapa nchini", amesema Abdul
Kutokana na uwepo wa rasilimali za kutosha hapa nchini lakini wananchi wake wanaishi maisha duni kwa kuwa rasilimali zimegeuka adhabu na laana kwa wananchi wake DP itahakikisha urithi wa watanzania utakuwa mikononi mwa wazawa wenyewe.
"Urithi wa rasilimali ulioachwa na waasisi wa Taifa ni lazima uwanufaishe watanzania mwekezaji anapokuja anapohitaji kuwekeza kipaumbele ni mchimbaji mzawa".
Uwepo wa madini ya aina mbalimbali hapa nchini kumekuwepo na wachimbaji wengi ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao na kujiongezea kipato na kujiletea Maendeleo.
Serikali ya DP itaweka utaratibu maalum utakaowezesha wachimbaji wadogo wadogo madini kuwa na haki ya kunufaika na madini wanayoyachimba kwa kupewa kipaumbele kwanza ndipo afuate mwekezaji,ubia umnufaishe mzawa kwanza.
Ameahidi kuondoa viwanja vya ndege vyote vilivyopo kwenye migodi kwa kuwa ni mojawapo ya viashiria vya wizi wa madini katika nchi.
"Watanzania tumeumbwa kuwa watu wa amani kwa nini tupoteze maisha kwa mali yetu ambayo Mungu ametupa ndio maana akayaweka madini nchini hayakuwekwa Ulaya".
DP itatengeneza Mazingira ya baadae kwa kuweka miundombinu ya ajira kwa Vijana kwa kufufua viwanda kwa kuwa rasilimali ni nyingi na malighafi zinapatikana hapa nchini,serikali madhubuti ni lazima ijenge uchumi imara kwa wananchi wake kwa kutumia rasilimali zilizopo kuleta Maendeleo.
Nchi hii imebarikiwa ardhi nzuri yenye rasilimali nyingi ambazo zikitumiwa kwa utaratibu mzuri zitawezesha upatikanaji wa huduma bora na kujenga uchumi imara kwa nchi na wananchi.
Ametolea mfano nchi ya Cuba inayotegemea zao la miwa pekee Kama rasilimali kubwa katika uchumi wa nchi hiyo lakini inatoa msaada hapa nchini kwa madai ya urafiki na ujirani mwema.
Katika kuweka usawa kwa watumishi wa Umma wanaostaafu kwa kuondoa mawazo DP itaondoa kikokotoo na kufanya maboresho ya kuweka Mazingira rafiki kwa wafanyakazi.
Abduli amesema"Kwenye serikali yangu mambo ya kwanza ni kufuta kikokotoo utafiti unaonesha kikokotoo hakipo kumsaidia mstaafu bali kipo kumsaidi mstaafu kufa haraka".
Kwenye serikali DP itaweka mkakati wa kugeuza kikokotoo kwa watumishi waliofanya kazi ndani ya mwaka mmoja ambao hawana utovu wa maadili kwa mujibu wa taratibu zilizopo kuwakopesha nyumba kwa kukatwa kidogo kidogo kwenye mshahara wake ili akistaafu awe na nyumba yake na atapewa fedha yake yote iliyobaki akatunze mwenyewe.
Kwa asilimia kubwa watumishi wengi wakistaafu ndipo wanakwenda kujenga huku kiwango alichopewa kuanza nacho ni kidogo hakikidhi mahitaji amesema Abdul.
Aidha amesema suala jingine atakalofanya ni kuboresha mishahara kwa watumishi waweze kuwa na morali ya uwajibikaji katika huduma wanazozitoa kwa wananchi kwa kuwa Mazingira ya kazi ni rafiki na watafanya kazi kwa starehe .
Amesema Tanzania ya Uhuru iliyoasisiwa na waasisi haifanani na Tanzania ya leo kwa sababu hivi sasa ujamaa umekwisha umebaki ubepari na ukabaila kuwepo kwa maskini na kumtaka abaki chini asinyanyuke kiuchumi huku ikirasimisha uchumi wake kwa wafanyabiasha wachache.
Serikali ya DP itafuata ndoto na nyayo za Rais wa awamu kwa kuweka usawa kwa wote na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kuwa na uzalendo utakaosaidia mzunguko wa fedha ubaki ndani kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.
Upande wa uvuvi atahakikisha anaweka utaratibu mathubuti kwa wavuvi kwa kupopeshwa zana za uvuvi zenye viwango vinakubaliwa tofauti na ilivyo.
"Serikali kupitia wizara ya fedha inakusanya kodi bandarini za nyavu halafu wavuvi wakinunua wanafilisiwa huu ni uonevu kwa watu wa hali ya chini DP itaondoa hilo,"amesema Abdul.
Hakusita kuonesha azma ya kuwachukulia hatua viongozi watakaobainika kuhujumu mali ya Umma bila kujali nyazifa zao
Amemalizia kwa kuwasihi wananchi kuhakikisha wanashiki uchaguzi ili kupata viongozi bora na kudumisha amani.




