Mgombea Urais kupitia CUF ahamasisha Watanzania wakapige kura

GEORGE MARATO TV
0


📌 Asema maandamano ni njia ya kuvuruga Amani ya nchi. 


Na MASHAKA MHANDO, Tanga 

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Gombo Semandito Gombo amewataka watanzania kutosusia uchaguzi mkuu kwani mabadiliko ya kweli yanatoka katika sanduku la kura.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu tathimini ya awamu ya kwanza ya kampeni za ugombea urais, ubunge na udiwani alizotembelea katika mikoa 14 aliyopita hapa nchini.

Amesema ni muhimu wapuuzie watu ambao wanafanya ushawishi wa kususia uchaguzi na kufanya maandamano ambayo yatasababisha kuvuruga amani iliyopo wakati amani iliyopo imeundwa na waasisi wa Taifa.

"Niwaombe watanzania jitokezeni kushiriki kwenye uchaguzi mkuu October 29 mwaka huu, kwenda kupiga kura ni haki yako ya msingi na ya kikatiba, sisi wapinzani tunatakiwa kushinda uchaguzi kwa njia ya amani na utulivu, nendeni mkapige kura," amesema Mgombea huyo Urais.

Alisema kuwa katika tathimini hiyo ya mikoa 14 aliyotembelea alisema kuwa kumekuwa na changamoto ndogo za kuingiliano wa ratiba hivyo akaotaka tume ya uchaguzi INEC kuondoka muingiliano huo ambao unaweza kuchafua na kutoa dosari uchaguzi ambao kimsingi amekiri zinakwenda vizuri.

Aidha amesema kuwa katika siku 100 atakapoingia Ikulu uongozi atahakikisha anaunda tume ya mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya ili kumaliza changamoto hiyo ambayo ni kilio cha watanzania kwa muda mrefu.

"Ndani ya siku 100 za uongozi wangu nitahakikisha nasimamia elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu sambamba na kudhibiti mianya ya rushwa.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top