Wasira: Dk. Samia Dereva Mzoefu Mpeni Usukani Atufikishe Pazuri

GEORGE MARATO TV
0


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema kwa miaka minne, Rais Dk,. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa hivyo Watanzania wanapaswa kumrudisha madarakani aendelee kuleta maendeleo mengi.

Wasira amesema hayo leo Septemba 27, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, mjini Moshi.

"Hapa Moshi kwa muda wa miaka minne amejenga shule mpya nne za msingi, sio kilimanjaro ni hapa hapa Moshi, amejenga madarasa mapya kwa sababu ya watoto kuongezeka 40, mjini hapa na nyinyi hamkuchangishwa.

"Kwenye afya amejenga zahanati tisa mjini Moshi, amejenga vituo vipya vya afya vitatu na amerekebisha hospitali na kuweka vifaa katika vituo vya afya na hospitali. Vituo vya afya vilivyojengwa chini ya Mama Samia ni kama hospitali tu, ukienda utakuta vifaa vyote vya hospitali viko mule.

"Kwa kufanya alivyofanya vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka 500 kwa vizazi 100,000 mpaka 100. Huyo ndiye Samia Suluhu Hassan," amesema.

Kuhusu huduma ya maji Moshi alisema yanapatikana kwa asilimia 100, hivyo hakuna tatizo la maji.

"Kwa hiyo Mama Samia kwa niaba ya Chama chetu ametekeleza wajibu wa kusaidia kuleta maendeleo.

"Sasa tunakwenda katika uchaguzi, hili ni ombi mahususi ambalo nalileta kwenu wananchi wa Moshi mjini na wa Kilimanjaro mkumbukeni na mpeni kura za kishindo Dk. Samia Suluhu Hassan. 

"Amefanya kazi kubwa na ilani hii mpya nayo ina mambo makubwa yanahitaji mtu mwenye uzoefu kusimamia na kusukuma maendeleo ya nchi yetu kutoka yalipo kwenda mahali mbele. 

"Wewe una gari jipya unatafuta dereva unachukua mtu hana leseni ataiangusha! Hana leseni unampa Scania aendeshe anasema huyu mimi ni ndugu yangu jirani, wacha ujirani uendelee lakini  kama sio dereva gari mkabidhi mwenye leseni. Samia ana leseni tena sio ndogo, kubwa," amesema Wasira.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top