DC Itunda amwakilisha RC mkutano wa Kimataifa

GEORGE MARATO TV
0


* Ni wa kujadili uhusiano wa maji, Nishati na Chakula


Na Mwandishi Wetu, Mbeya

MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa, katika Mkutano wa Kimataifa wa nchi tisa uliojadili namna bora ya kuunganisha rasilimali za maji, nishati na chakula ili ziweze kumnufaisha binadamu.

Mkutano huo wa kihistoria umefanyika Jijini Mbeya ambapo uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Itunda alisisitiza kuwa rasilimali za maji, nishati na chakula zinapaswa kutazamwa kwa jicho la pamoja kwani zinategemeana kwa kiasi kikubwa. 

Alieleza kuwa mustakabali wa maendeleo endelevu ya jamii yoyote hauwezi kufikiwa endapo uhusiano kati ya sekta hizo hauzingatiwi kwa pamoja katika sera, mipango na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkutano huo umehusisha wataalamu wa ndani na nje ya nchi kutoka mataifa tisa waliobadilishana uzoefu, tafiti na mbinu bunifu juu ya jinsi rasilimali hizo tatu zinavyoweza kuunganishwa ili kusaidia jamii kupata huduma bora za maji safi, nishati endelevu na chakula cha uhakika. 

Pia, DC Itunda alitoa tahadhari kwa kuhakikisha washiriki hao wanazingatia athari za mabadiliko ya tabianchi, usimamizi shirikishi wa rasilimali, na uwekezaji wa kiteknolojia kwa ajili ya uzalishaji wenye tija.

Katika mkutano huo, Mhe. Itunda alitoa wito wa kuongeza uwekezaji katika tafiti, teknolojia rafiki kwa mazingira na mikakati ya pamoja ya kikanda ili kuhakikisha maji, nishati na chakula vinapatikana kwa usawa, uhakika na uendelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Nchi zilizohudhuria mkutano huo ni pamoja na Tanzania ambaye ndio mwenyeji, Israel, Marekani, Malawi, Ethiopia, Kenya, Zambia, Botswana na  Uganda. 








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top