Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Watano Wahukukiwa Kunyongwa Hadi Kufa


 Na Angela Sebastian ;Bukoba

MAHAKAMA kuu kanda ya Bukoba imewahukumu watu watano kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauji ya kukusudia Wilayani Ngara mkoani Kagera kwa  nyakati tofauti.

Wakili wa Serikali Grolia Lugeye akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mashtaka mjini Bukoba amesema katika tukio la kwanza lilitokea Novemba mosi,2018  majira kati ya saa sita hadi saba usiku kitongoji cha Kukazulu kijiji Mulugalama Wilayani Ngara  ambapo washitakiwa Julius Ngeze (55),Jackson Bwelele (47) na Seleman Lwandindi waliwaua watu wawili mme na mke.

“Siku ya tukio majira ya usiku washitakiwa hao walienda nyumbani kwa Amosi Mfumu (80) ambaye ni marehemu na kuvunja mlango na baada ya kuingia ndani walikutana na mgeni ambaye alilala sebureni aliyejulikana kwa jina la Mibulo Benedicto na kumuweka chini ya ulinzi ,wakati huo marehemu Amosi baada ya kusikia purukushani alitoka chumbani ndipo akakutana na wauaji hao na kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufa”ameeleza Lugeye.

Amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo waliingia chumbani na kumuua pia mke wa marehemu Amosi ambaye aliitwa Solina Amosi (43) na kisha wakaiba simu ya Mibulo ambaye alikuwa mgeni na kutokana na taa za mwanga wa jua zilizokuwa zikiwaka ndani Mibulo aliweza kuwatambua washitakiwa hao na kisha kutoa taarifa kwa majirani ambao walitoa taarifa kituo cha polisi  na kufanikiwa kukamatwa.

Amesema kesi iliendelea kusikilizwa ambapo chanzo cha mauaji ni kwamba marehemu Amosi alihifadhi ng’ombe wake kwa Selemani Lwandindi ambapo alimtaka amrejeshee mifugo yake ndipo akajibiwa kuwa watarejeshewa lakini Selemani hakufanya hivyo badala yake aliwatafuta wauaji hao ambao ni Julius Ngeze,Jackson Bwelele na mwingine aliyeitwa Sadick alifariki wakati kesi ikiendelea.

Mahakama kuu kanda ya Bukoba ilisikiliza pande zote mbili na kulidhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri bila kuacha shaka lolote kuwa walifanya mauaji ya kukusudia ndipo ikawatia hatiani washitakiwa wawili ambao ni Julius Ngeze na Seleman Lwandimdi na kuhumumiwa kunyongwa hadi kufa huku Jackson Bwelele akiachiwa huru kwani alitajwa na wenzake na mahakama iliona ushahidi dhidi yake haukujitosheleza.

Hukumu hiyo ilitolewa Juni 13 mwaka huu na jaji Lilian Itemba jaji wa mahakama kuu kanda ya Bukoba ambapo mawakili upande wa utetezi walikuwa ni Grolia Lugeye,Matrida Assey na Alice Mutungi ambao ni mawakili wa Serikali.

Katika tukio la pili Wakili Alice Mutungi amewataja washitakiwa Renatusi Misigalo (51),Mwendapole Andrea (44) na Kalenzo Ruhinda maarufu Ngaramandaje (54) wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua David Mbilahisha (52)kwa kukusudia.

“Washitakiwa hao walitenda kosa mnamo Januari 30,2017 katika kijiji cha Rulenge Wilayani Ngara ambapo siku hiyo majira ya usiku washitakiwa walifika nyumbani kwa David ambaye ni marehemu na kugonga mlango wakiwa na silaha zenye ncha kali ikiwemo panga huku,wakimuita mtoto wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Dickson David wakimtaka awafungulie mlango ambapo marehemu alitambua sauti ya Renatusi kwa kuwa walikuwa wanaishi kijiji kimoja na kwenda kumfungulia”ameeleza Mutungi

Amesema baada ya kufungua mlango washitakiwa walimuweka David chini ya ulinzi na kumfunga kamba mikono na miguu,pia wakawachukua watoto watatu wa familia hiyo wakawafunga kamba mikono na miguu na kisha wakamuamuru marehemu awapatie fedha kwa sababu alikuwa ameuza shamba.

 Amesema marehemu aliwajibu kuwa hana fedha ndipo wakaanza kutafunta wenyewe vyumbani na hawakupata chochote,wakaanza kumshambulia kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufa baada ya kuona kafa waliiba televisheni moja na simu tatu za mkononi kisha kutokomea lakini watoto waliweza kuwatambua washitakiwa hao na walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge na washitakiwa kukamatwa.

Amesema Mahakama kuu kanda ya Bukoba baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka pasipo kuacha shaka lolote iliwatia hatiani washitakiwa  hao wote watatu kunyongwa hadi kufa ambapo hukumu hiyo ilitolewa Juni 13,mwaka huu na jaji Lilian Itemba jaji wa mahakama hiyo huku upande wa mawakili wa Serikali walioenedesha kesi hiyo wakiwa ni Agnes Awino,Grolia Lugeye na Alfred Tairo.

Katika tukio la tatu Wakili wa Serikali Alfred Tairo amesema mnamo Aprili 10,2024 katika kijiji cha Kilima Wilaya ya Bukoba ambapo Jovinary Godwin maarufu Muganyizi (16) na Editha Hermany maarufu Koku (47) walishitakiwa kwa kumuua mtoto Elias Antony (11) mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kilima ambapo siku ya tukio marehemu alikuwa na baba yake shambani wanachoma mkaa ambapo baba wa marehemu alimtuma mtoto aende nyumbani kuchukua unga,fedha na kisha apitie dukani ambapo baba aliacha simu kwa ajili ya kuongeza umeme.

“Marehemu alifanya kama alivyoelekezwa na baba yake lakini alichukua muda mrefu bila kurudi ambapo baba alimfuatilia bila mafanikio,Aprili 11 mwaka jana mwili wa marehemu ulipatikani ukiwa umekatwa na  kitu chenye ncha kali shingoni ukiwa umetupwa kwenye eneo la tingatinga ambapo walifanikiwa kumkamata mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Jovinary ambapo alikiri kutekeleza mauaji hayo na kumtaja mshitakiwa wa pili Editha”ameeleza Tairo

Amesema baada ya jaji Lilian Itemba wa mahakama kuu kanda ya Bukoba kusikiliza ushahidi uliotolewa alitoa hukumu ambapo Jovinary alipatikana na hatia lakini kwakuwa ni mtoto hakuhukumiwa kunyongwa amerudishwa rumande mpaka Waziri wa katiba na sheria atakavyoona inafaa huku mshitakiwa wa pili Editha akiachiwa huru kutokana na ushahidi uliotolewa na mshitakiwa wa kwanza haukujitosheleza.





Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...