Ufunguzi wa Michuano ya kandanda kwa wachezaji wa ndani barani Afrika(CHAN)Kwa mwaka 2025 utafanyika Jijini Dar-es-laam katika uwanja wa mkapa August 2.
kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imeeleza kuwa shirikisho la kandanda barani Afrika(CAF)Tayari imemjulisha Waziri Prof.Palamagamba Kabudi kuhusu uamuzi wa Dimba la Mkapa kuwa mwenyeji wa ufunguzi wa michuano ya CHAN.
Kufuatia uamuzi huo,Waziri Kabudi ametoa wito kwa wadau wote kuchangamkia fursa mbalimbali zinazoambatana na kufanyika kwa mashindano hayo Nchini ikiwemo biashara za bidhaa mbalimbali,huduma za usafiri,utalii na kuvutia uwekezaji.
Michuano ya CHAN inatarajiwa kuanza Juni 2 hadi 28 mwaka huu hadi katika vituo vinne ambavyo ni Dar es salaam,Zanzibar,Nairobi(Kenya) pamoja na Kampala(Uganda)
Michuano ya CHAN 2025 yatafuatiwa na michuano ya AFCON 2027 ambapo mataifa ya Tanzania,Kenya na Uganda yatakuwa wenyeji.

Comments
Post a Comment