Msajili wa Vyama Vya Siasa Ana Mamlaka ya Kutengua Uteuzi wa Chama Chochote Cha Siasa Kwa Mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni
Na David Maphone.
Nimemsikiliza vizuri Makamu Mwenyekiti Mhe, John Heche, Katibu Mkuu John Mnyika pamoja na Mjumbe wa Baraza kuu la Chadema Godbless Lema kwa nyakati tofauti wakipinga maamuzi ya Msajili wa vyama vya siasa. KUTENGUA Uteuzi uliofanywa KIMAKOSA na Baraza kuu la Chadema 2025 Mlimani city D'Salaam.
Lakini pia nimewasikiliza baadhi ya wanasheria wao wakidai Kwamba Msajili wa vyama hana mamlaka ya Kisheria KUTENGUA UTEUZI wa Chama Cha siasa .
Kwa kuwa suala hili limetolewa Kauli pia na wanasheria wa Chadema na Mwanasheria William Maduhu wa LHRC kwa UPOTOSHAJI huu nimeona muhimu Watanzania wafahamu ukweli wa uongo huu.
Kwa mujibu wa Sheria ya vyama vya siasa Sura Namba 258 Ibara 22 (1)"The Minister may make regulations for the purpose of carrying out OR giving effect to any PROVISION of this Act."
Kwa kuwa Ofisi ya Msajili wa vyama ipo kwa mujibu wa Katiba, Sheria na KANUNI na tumeona hapo juu.
Kanuni zipo kwa mujibu wa Sheria. Ibara 22 (1) hivyo basi, Mamlaka ya Msajili wa vyama KUTEGUA uongozi yapo kwenye Kanuni ya 31 (2) kanuni ya usajili na ufatiliaji wa vyama vya siasa inampa mamlaka msajili wa vyama kukataa au kukubali mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Chama Cha siasa.
Msajili anaweza kukataa mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Chama Cha siasa endapo hayajafanywa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, katiba na kanuni za Chama husika.
Natoa mwaliko kwa wanasheria na viongozi wa Chadema kusoma Kanuni 31(3) Msajili atakataa mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Chama na atakielekeza Chama husika kutekeleza matakwa ya sheria ya vyama vya siasa kwa kuteua/kuchagua Viongozi kwa kufata sheria katiba na kanuni ZAO na kuwasilisha tena.
Kama kuna watu wanapaswa kujivuna kwa jamii ni wanasheria mpaka wamefikia kujiita "WASOMI" kama utambulisho wao hii ni kutokana na Kufanya Utafiti kabla ya Kufungua mdomo.
Ni Aibu kwa kwa Wakili msomi kutoa Kauli zake bila Kufanya "HOMEWORK" ya kutosha.
Nimesikitika sana kwa Wakili msomi William Maduhu kwa alicholisema sasa nampa mwaliko kusoma Kifungu Cha 4(5)(a) msajili ndiyo mwenye mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa sheria ya vyama.
6A(2) Chama lazima kiendeshwe kwa kufata katiba yake.
Ushauri wangu,
Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema kupanga ni kuchagua.
Chadema Wana mambo MATATU muhimu ya kuchagua kwenye sakata hili.
1. Kwenda Kufungua Shauri Mahakamani kupata tafsiri ya Kisheria kuhusu mamlaka ya Msajili kuhusu KUTENGUA.
2. Kufuata Maelekezo ya msajili wa vyama kama walivyoelekezwa kwenye barua.
3. Kukomaza shingo ili kusubili hatua Kali zaidi ambazo sio njema kwa Afya ya Chama Chao.
Kwa muktadha huo machaguo sahihi ni kwa Uongozi wa Chadema waliopo madarakani kwa sasa.
Narudi tena
Mwandishi
David Maphone
Dsm Tanzania.

Comments
Post a Comment