Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha kadi yake ya mpiga kura mara baada ya kushiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma ambapo pia aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari hilo.
Mapema Rais Samia alitumia usafiri wa Treni ya SGR kutoka Dar es saalam hadi Dodoma kuja kushiriki katika zoezi hilo ili aweze kupata haki yake ya msingi ya kupiga Kura katika uchaguzi unatarajiwa kufanyika badae mwaka huu wa Madiwani,Wabunge na Rais

















Comments
Post a Comment