Na Ada Ouko, Dodoma.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Mpango leo mei 17 mwaka 2025 ameondoka nchini kuelekea Nchini Brazil kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa pili unaohusu usalama wa chakula, mapambano dhidi ya njaa na maendeleo vijijini.
Mkutano huo wa pili wa Brazil na Afrika unatarajia kufanyika jijini Brasilia kuanzia tarehe 20 hadi tarehe 23 Mei mwaka huu 2025.
Aidha mkutano huo utawakutanisha viongozi, wakuu w nchi na serikali, Mawaziri wa kilimo kutoka Afrika, Mashirika ya kimataifa, Benki ya Dunia pamoja na watalaamu mbalimbali.
Sambamba na hilo Makamu wa Rais pia anatarajiwa kushiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania Mashirika na Mataifa yanayoshiriki mkutano huo.

Comments
Post a Comment