Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel M. Maneno na Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius J. Njole wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa Mkutano wa Kumi na Tisa, Kikao cha Kumi na Tano cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria inatarajiwa kuwasilishwa katika Kikao hicho cha Bunge leo tarehe 30 Aprili, 2025.
#BajetiyaWizarayaKatibanaSheria