Na Shomari Binda-GMTV
SHEREHE za ufunguzi wa shule mpya 4 za sekondari zinatarajiwa kufanyika jimbo la Musoma Vijijini kuanzia aprili 24 hadi 29,2025 huku wanafunzi,walimu,wazazi na wadau wa elimu wakikaribishwa.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amewakaribisha na kudai hilo ni tukio muhimu na kubwa kwa maendeleo ya elimu.
Akizungumza na GMTV leo ijumaa aprili 18,2025 Muhongo amesema ratiba itaanzia Butata sekondari iliyopo Kijijini Butata Kata ya Bukima siku ya alhamisi aprili 24,2025 kuanzia saa 6:30 mchana mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka.
Amesema ijumaa aprili 25 itakuwa ratiba ya sekondari ya Kumbukumbu ya David Massamba Kijijini Kurwaki Kata ya Mugango kuanzia saa 6:30 mchana
Muhoji sekondari iliyopo Kijijini Muhoji Kata ya Bugwema itafunguliwa Jumatatu aprili 28 kuanzia saa 6:30 mchana huku Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi akiwa mgeni rasmi
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na mbunge huyo Nyamrandirira sekondari ya Amali iliyopoKijijini Kasoma Kata ya Nyamrandirira itafunguliwa jumanne aprili 29 kuanzia saa 6:30 mchana
Aidha mbunge Prof.Muhongo amesema licha ya kufunguliwa sekondari hizo 4 ujenzi wa sekondari nyingine unaendelea kwenye vjijini vya Nyasaungu Kata ya Ifulifu, Kisiwani Rukuba Kata ya Etaro, Kijijini Mmahare Kata ya Etaro,Kiriba Kata ya Kiriba,Kataryo Kata ya Tegeruka,Nyambono Kata ya NyambonoMusanja, Kata ya Musanja na Chitare Kata ya Makojo
" Idadi ya sekondari kwenye Kata 21 zenye vijiji 68 ni 26 za serikali na 2 za binafsi tunakwenda kufungua hizi 4 na kuongeza idadi ya shule.
" Tunaendelea kuwakaribisha wadau wa elimu kuja jimboni mwetu kuchangia ujenzi wa shule zikiwemo za awali( shikizi),msingi na za sekondari",amesema.