Rpc Mara Atoa Angalizo Kwa Watumiaji wa Barabara Kuelekea Sikukuu ya Pasaka

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

KAMANDA waPolisi mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Pius Lutumo ametoa angalizo kwa watumiaji wa barabara kuwa makini na waangalifu katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka.

Akizungumza na GMTV kwa njia ya simu leo aprili 18,2025 kuelekea sikukuu hiyo amesema kila mtumiaji wa barabara wakiwemo madereva na watumiaji wengine kuongeza umakini ili kuepuka ajali.

Amesema madereva wa magari,pikipiki na vyombo vingine vya moto wasitumie pombe wanapokuwa wanaendesha kwani ni kisababishi cha ajali.

Kamanda Lutumo amesema jeshi la polisi limeimalisha ulinzi na litawachukulia hatua kali wale wote watakaokamatwa kwa kwenda kinyume na matumizi sahihi ya barabara.

Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mara amewasisitiza madereva kuacha miemko na kuwajali watumiaji wengine wa barabara ili washerehekee sikukuu kwa amani.

Amesema chanzo cha ajali nyingi imekuwa ni pamoja na uzembe na matumizi ya vileo na kupelekea vifo na ulemavu na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

" Nitoe tahadhari kwa watumiaji wa barabara wote wakiwemo madereva na waenda kwa miguu katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka.

" Jeshi la polisi limeimalisha ulinzi zaidi na litakuwa na doria kali kwenye makazi ya watu na nyumba za ibada na kuwa na oparesheni maalum barabarani na nitoe onyo kwa dereva yoyote kuacha kutumia kilevi na kuendesha chombo cha moto.

" Maeneo ya ibada ulinzi utaimalishwa wakati wote wa ibada muanzia mkesha wa Pasaka ili kila mmoja asherehekee sikukuu kwa amani na utulivu na yoyote atakayepanga kufanya vitendo vya uhalifu ataishia mikononi mwa polisi",amesema.

Aidha kamanda Lutumo ametoa wito wa wazazi na walezi kuwa makini na watoto na kuacha tabia za kuwaacha wenyewe nyumbani bila uangalizi na wanapokwenda kwenye maeneo ya beach.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top