Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) leo tarehe 18 Aprili, 2025 imekabidhi Taulo za Kike (Sanitary Pads) 350 kwa Wasichana walio katika mazingira magumu nyakati za hedhi husababisha changamoto kubwa kwa wasichana kuhudhuria masomo yao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) Mhe. Sabra Ali Mohamed amekabidhi Taulo za kike (Sanitary Pads) 350 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Zanzibar Ndugu Siti Abasi Ali, ili kuweza kugaiwa kwa Madawati ya Jinsia ambayo yapo kwenye masoko na bandari na Dahalia za Shule zilizopo Pemba.
Vilevile, Mhe. Sabra Ali Mohamed amekabidhi Taulo 150 kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) - Zanzibar ili kuweza kugaiwa kwa Shule za Mikoa yote ya Unguja. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za MIF zilizopo Mazizini - Unguja.