OFISI ya mwanasheria mkuu wa serikali imechukua hatua ya kutekeleza agizo la MH. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania MH. DK SAMIA SULUH HSSAN la kujiimarisha kisheria kuwaongezea uwezo watendaji wake katika majadiliano na usimamiziwa mikataba inayoingia baina ya serikali na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi kwa kuitisha mafunzo maalumu ya siku tano yatakayohusisha mawakili mia tatu wa serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari kwake leo mach.19. mwaka huu 2025 Mwanasheria mkuu wa serikali MH. HAMZA JOHARI amesema mafunzo hayo ya siku tano takayofanyika jijini Arusha kuanzia mach. 24 na kuendeshwa na wakufunzi wa ndani na nje ya nchi yatashirikisha maawakili wa serikali kutoka ofisi hiyo, wizara, taasisi, idara na mamlaka za serikali za mitaa nchini kote.
Kwa sababu hiyo Mh. mwanasheria mkuu wa serikali amewataka waajiri katika wizara, idara taasisi na mamlaka za serikali za mkitaa kutoa ruhusa kwa mawakili wao ili waweze kushiriki katika mafunzo hayo muhimu.
Mwanasheria mkuu wa serikali ametumia mkutano huo kutoa pongezi kwa Rais MH. DK. SAMIA SULUH HASSAN kwa kutimiza miaka minne ya uongozi wake ambapo amesema katika kipindi hicho taifa limepata mafaniko makubwa katika sekta mbalimbali.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo psmoja uingiaji mzuri wa mikataba hatua ambayo imewezesha kupata mafanikio hayo.
















Comments
Post a Comment