Wavuvi 540 Waokolewa, 10 Wanatafutwa Ziwa Rukwa

GEORGE MARATO TV
0


Wavuvi 540 waliokuwaa wanafanya shughuli za Uvuvi katika Ziwa Rukwa wameokolewa na Wavuvi 10 wanaendelea kutafutwa kufuatia upepo mkali uliotokea mnamo tarehe 23 Januari 2025 katika ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amefika Kata ya Nankanga kuungana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji kujionea kazi ya uokozi huku akiwa ameambata na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga pamoja na Askari Wazamiaji.

Kwa Upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji ametoa pongezi kwa Wananchi kwa kushiriki kikamkalifu katika uokoaji pamoja na kutoa ushirikiano wa kuwatambua wavuvi wengine ambao walikuwa hawajasajiliwa katika Vikundi na makampuni.

Mkuu wa wilaya ya Sumbwanga Nyakia Chirukile ameelewa kuwa mnamo tarehe 23 Januari 2025, Jumla ya Wavuvi 550 kutoka Kata ya Nankanga na Mtowisa waliokuwa wanaendelea na shughuli za Uvuvi katika ziwa Rukwa walipatwa na dhoruba ya upepo mkali katika Ziwa Rukwa.

Akitoa salama za Pole, Waziri Bashungwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kupata taarifa hizo, ametoa helkopta ya Jeshi iliyoambatana na Wazamiaji na vifaa maalum za uokozi ili kuongeza nguvu za Uokoaji







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top