
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, amewasilisha ombi hilo kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Magu, baada ya mbunge wa jimbo hilo Desdery Kiswaga kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho, mbunge wa jimbo la Magu Desdery Kiswaga, amesema jimbo la Magu katika kutekeleza limepokea shilingi bilioni 143, zilizoelekezwa katika miradi huduma muhimu za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji, barabara
Kuhusu miradi ambayo bado haijakamilika, mbunge huyo amesema inaendelea kutekelezwa kwa kasi.
Wanachama wa CCM na wananchi, baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama, kwa kauli moja wameridhia tamko la utekelezaji wa miradi mbalimbali, huku wakiahidi kuendelea kukiunga mkono Chama cja Mapinduzi kwa kulopatia kura za kutambua uwajibikaji.