Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo ametembelea Makumbusho ya Louvre iliyoko Abu Dhabi katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)
Mhe. Waziri Kombo ametembelea Makumbusho hayo ambayo ni jumba la sanaa lililopo kwenye Kisiwa cha Saadiyat jijini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu tarehe 03 Desemba, 2024 na kujionea jinsi jumba hilo lilivyohifadhi na kuelimisha kwa namna ya kipekee katika mazingira ya kisasa inayodhihirisha na kutafakarisha juu ya utawala, maarifa na ustadi wa ufundi wa utamaduni wa watu na viongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Makumbusho ya Jumba hilo la Louvre inaendeshwa chini ya makubaliano kati ya UAE na Ufaransa yaliyosainiwa Mwaka 2007, yanayoruhusu kutumia jina la Louvre hadi mwaka 2047.
Makumbusho ya Louvre inaelezwa kuwa ni mradi mkubwa zaidi wa kitamaduni wa Ufaransa ulioko nje ya nchi hiyo.







Comments
Post a Comment