Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,Ajira na wenye ulemavu Mh Ridhwani Kikwete,amepata nafasi ya kumsindikiza Mh. Dotto Biteko , Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwenye uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa Watu Wenye Ualbino ( MTHUWWU) na Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar Es Salaam.
Mipango hii miwili ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, maelekezo na ahadi ya Mh. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa akihutubia Bunge kuhusu kuwalinda watu wenye Ualbino nchini. #KaziInaendelea





Comments
Post a Comment