Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, amekutana na kufanya mazungumzo na mawakala wa forodha katika mpaka wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, tarehe 28 Novemba 2024, ofisini kwake iliyopo Nselewa, wilayani Mbozi.
Katika kikao hicho, Mhe. Chongolo ametoa wito kwa mawakala wa forodha kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuwasababishia fedheha. Aidha, mesisitiza na kuacha na na vitendo vitakavyo waingiza matatani
Mazungumzo hayo yamelenga kutafuta suluhisho la changamoto za foleni za malori katika mpaka wa Tunduma, ambazo zimekuwa zikiathiri ufanisi wa shughuli za forodha na usafirishaji. Mkuu wa Mkoa amehimiza ushirikiano wa dhati baina ya wadau wote katika kuboresha huduma mpakani na kuimarisha uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Kikao hicho kimehudhuriwa na mawakala wa forodha na wadau wengine wa forodha, ambao walipata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu changamoto zinazowakabili.





Comments
Post a Comment