Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC)imehimiza Waandishi wa Habari Kupewa Ushirikiano wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 Mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mpc Edwin Soko katika Taarifa yake kwa Umma.
‘’Mpc imetoa rai kwa wadau wa uchaguzi mkoa wa mwanza kuwapa ushirikiano wa kutosha waandishi wa habari wote watakaokuwa kwenye mbalimbali wakitekeleza majukumu yao,Kwa kuwa Waandishi wa habari wana wajibu wa kikatiba wa kutafuta,kuchakata na kutoa taarifa kwa umma kupitia ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ilieleza Taarifa ya Soko.
Mwenyekiti huyo wa Mpc ameeleza matarajio yake kuwa wadau wote wa uchaguzi watatoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa Habari huku akilikumbusha Jeshi la polisi kuendelea kuwalinda raia wote wakiwemo wanahabari wanapotimiza majukumu yao.
Aidha amewataka waandishi wa habari kuvaa Press Jackets(Vizibao)ili waweze kutambuliwa kwa urahisi na wadau watakapokuwa wanatekeleza majukumu yao