MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara mh Ghati Chomete,amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ambayo pia yamewezesha watoto wa masikini wakiwemo watoto wa kike kupata elimu hiyo bila vikwazo.
Mh Chomete ameyasema hayo leo Novemba 15-2024 wilayani Tarime wakati akishiriki kampeni ya "Tunasimama na Mama Samia Binti Abaki Shuleni" kwa kuwagawia Taulo za kike kwa lengo la kulinda hedhi salama.
Amesema katika mageuzi hayo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Samia ni pamoja na ujenzi wa shule mpya zikiwemo za watoto wa kike,miundombinu ya elimu,kutatua changamoto zikiwemo za upandishwaji wa madaraja kwa walimu hatua ambayo imewezesha kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu mkoa wa Mara na taifa kwa ujumla.
Kwa sababu hiyo amewata wanafunzi hao wa shule ya Sekondari ya Tarime Bomani na Iganana kusoma kwa bidii katika kuunga mkono jitihada hizo kubwa za Rais Samia na kwamba Serikali itaendekea kuwawekea mazingira mazuri ya kujifunzia hasa kwa masomo ya Sayansi.
Mbunge huyo mbali na kuendesha kampeni hiyo pia amesisitiza kuwa jamii kuachana na mila na desturi zinazochangia ukatili kwa mtoto wa kike.
Kuhusi uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novembe 27 mwaka huu,mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Mara amewataka wanafunzi ambao wamejiandikisha kujitokeza siku ya kupiga kura ili kutimiza haki yao ya msingi kuchagua viongozi wanaweza kusimamia miradi na fedha zinazolewa na Serikali ya CCM kutekeleza miradi katika maeneo yao.
Katika kampeni hiyo ya kugawa taulo hizo za kike, mbunge huyo pia amegawa mipira na Michele kilo 150 kwa shule hizo.




