Serikali yawapa Uhakika Wajasiriamali Wanawake

GEORGE MARATO TV
0


SERIKALI imewahakikishia Wajasiriamali Wanawake na Vijana kuwa itaendelea kuwawezesha kwa kuwapatia maarifa, masoko, fursa za kijamii na kiuchumi ili waweze kupiga hatua katika kujenga uchumi wa familia na jamii kwa ujumla. 

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi,ajira na watu wenye Ulemavu Mh Ridhwani Jakaya Mrisho Kikwete,ametoa msimamo huo wa Serikali jijini Dar es Salaam jana Novemba 15 mwaka 2024 wakati akizindua jukwaa la soko la bidhaa zinazozalishwa wajasiliamali wazawa.

Kupitia jukwaa hilo la Wajasiliamali wazawa Wasichana na vijana wa Panda linaloratibiwa na taasisi ya Her Initiatives chini ya uongozi wa bi Lydia Thomas,waziri huyo wa nchi mwenye dhamana ya kazi na vijana amesema serikali inaamini ukisaidia makundi haya muhimu itakuwa umesaidia Jamii. 

Taasisi hiyo inajulikana kutokana na juhudi kubwa inazofanya duniani kwa kuwanyanyua vijana na Wanawake na kuwezesha wameshinda zawadi za Utambuzi maeneo mengi ikiwemo ile ya Global Citizen inayotolewa Marekani na ile inayotolewa na Mfalme wa Ubelgiji.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top