Mtendaji Mkuu Tarura Mhandisi Victor Seif amwagiza Mkandarasi Kukamilisha Ujenzi wa Nguzo Mbili za Daraja Zilizobakia Kabla ya Msimu wa Mvua Kuanza

GEORGE MARATO TV
0



*Rufiji, Pwani.*

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) amemtaka Mkandarasi MAC Contractor Ltd anayejenga Daraja la Mohoro lililopo Wilayani Rufiji  Mkoa wa Pwani kukamilisha ujenzi wa nguzo mbili zilizobakia  kwenye ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa mvua za msimu zinakaribia. 

Alisema, ujenzi wa nguzo hizo utapelekea utekelezaji wa Mradi kwa hatua inayofuata kutokukwama wakati wa Mvua.

Agizo hilo amelitoa tarehe 15.11.2024 aliporudi tena kwa mara ya pili  ikiwa ni ahadi aliyoitoa wiki iliyopita alipoutembelea mradi huo.

Mhandisi Seff, amemtaka Mhandisi  Mshauri  wa TREECO Mhandisi Emmanuel Mahimbo kumsimamia Mkandarasi  MAC ili amalize kazi kwa Wakati.

Mhandisi Mahimbo alieleza kuwa tatizo kubwa la Mkandarasi ni kutokua na malighafi za Ujenzi kama Cement hivyo kupelekea baadhi ya kazi kusuasua.

Vile vile Mhandisi Seff  alitembelea  kwa mara ya pili Mradi wa  Ujenzi wa Barabara ya Utete-Kingupira (32km) inayojengwa kwa Kiwango cha  Changarawe kwa kutumia Teknolojia Mbadala ya ECOROADS na Mkandarasi NRST LIMITED CIVIL WORKS CONTRACTOR JV DASHAS COMPANY LIMITED

Mhandisi Seff hakuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi huo na kumuelekeza Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Rufiji Mhandisi Nicolaus Ludigery kuhakikisha Mkandarasi NRST awasilishe programu ya kazi inayoonesha namna atakavyofidia siku zilizopotea na kukamilisha kazi kwa wakati, vinginevyo hatua za kimkataba zitachukuliwa.

Mradi  wa ujenzi wa barabara ya Utete-Kingupira umepangwa kukamilika mwezi Aprili 2025.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top